Wanajeshi wa Kimarekani zaidi ya 3000, wapo katika mafunzo ya kijeshi
huko Sattahip, Thailand yanayohusisha kunywa damu ya nyoka aina ya Cobra
na kumchinja kuku hai kwa mdomo.
Wanajeshi hao wa jeshi la Wanamaji na mabaharia walioshiriki mafunzo ya
siku kumi walifanya jaribio la kukata kichwa cha kuku mzima kwa mdomo na
wanyama wengine jamii ya reptilia.
Kiongozi wa Jeshi la Wanamaji, Harry B. Harris alisema katika taarifa
yake kuwa mafunzo hayo yanajumuisha namna ya kukabiliana na wanyama wa
porini, kujihami na wanyama mazoezi makali ya moto.
“Kunywa damu ya cobra ni sehemu ya mafunzo ya kukabiliana na mazingira ya porini.” alisema Harris
Pamoja na Marekani, nchi nyingine zilizoshiriki katika mafunzo hayo
makali ni Thailand, Singapore, Japana, Indonesia na Malaysia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni