Hapa anahojiwa moja wa kada wa CHADEMA ambae yupo moja kwa moja kwenye eneo la tukio mjini Arusha kama ifuatavyo,
"Baada ya maswali mazito na hoja ngumu kumeza kutoka kwa mawakili wetu, hiki kimetokea kwa mawakili wa serekali. Wakili wa Serikali aliomba dk 15 kuwasilisha hoja na Wakili Msomi Peter Kibatala amekubali na kuomba wapewe saa 1 kujibu so Mahakama ikaahairishwa mpaka saa 7 mchana. Mji wa Arusha mda huu umesimama ikiwa ni siku ya kuletwa mahakamani kwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema, Ninaposema umesimama namaanisha kwamba maeneo ya Mahakama na eneo la Uzunguni watu wamejaa sana baada ya kufika mahakamani na kufukuzwa, Kwa macho yangu nimeshuhudia magari ya Wabunge zaidi ya 20 wakifika mahakamani na magari yao kuzuiwa getini na kutakiwa kuingia Mbunge kama Mbunge, Pia nimeshuhudia Viongozi wakitaifa wajumbe wa kuu ya Chama wakiongozwa na Mwenyekiti Mboye, Mjumbe wa kamati kuu Edward Lowasa, Waziri mkuu mstaafu Sumae na wengine wengi msafara wa magari ya kamati kuu Yameruhusiwa kuingia ndani ya mahakama, Baada ya msafara huo kufika wananchi walianza kupiga kelele huku wakiimba Raisi raisi raisi raisi huku polisi wakiona na wakisikia wimbo huo ukiimbwa kwa mbwembwe nyingi...... Hadi sasa ninapoandika nip jirani na mahakama nikiangalia kwa mbali kinachoendelea, Hali ya Arusha ni yabaridi mda huu na story za siasa zikiwa zinapigwa kila kona. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Godbless Lema.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema".
Tutaendelea kuwaletea taarifa kadiri ya uwezo wetu kwa kile kinachoendelea baada ya Mh. Lema kupata dhamana hii leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni