Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amedai kuwa
kada wa Chadema, Anitha Kimario (44) aliyeuawa alikuwa awe shahidi
katika kesi moja dawa za kulevya.
Mutafungwa amesema kiini cha mauaji hayo kinachunguzwa.
Shauri hilo linamhusisha kinara wa usafirishaji wa bangi kwenda nchini
Kenya, kupitia njia za panya zilizopo mpakani wilayani Rombo.
Kamanda Mutafungwa amesema polisi wanachunguza mazingira ya mauaji hayo
ili kubaini waliohusika, huku akisema watu wawili wanashikiliwa kwa
mahojiano.
Mutafungwa amesema juzi jioni polisi waliokota mwili wa mwanamke huyo
ambaye pia ni mfanyabiashara ukiwa umetupwa kwenye mashamba ya miwa.
“Tulipofika eneo la tukio tulikuta mwili wake ukiwa umewekwa kwenye
matuta ya kupandia miwa ukiwa umefunikwa na majani na udongo, umevuliwa
nguo na kubaki na za ndani,” amesema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni