Jeshi la Polisi Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vennesa Mdee
maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.
Mwanasheria wake Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake
amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati akitaja majina ya
wanaojihusisha mwezi uliopita.
Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini
kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza Polisi
walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa
Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka
1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye
Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume
Challenge na baadae kidogo wakati ananza alikuwa chini ya Lebo B'hitts.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni