Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na wizi, uuzaji na ununuzi wa mafuta ya ndege nchini.
Kamanda wa kanda maalumu afande Kamishna Simon Sirro |
Kamishna Sirro ametoa onyo hilo leo jijini Dar es Salaam baada ya kumkamata mttu mmoja aitwae Iddy Juma Nyangasa mkazi wa Vingunguti baada ya kuiba lita 38 za mafuta ya ndege kutoka kwenye ndege mali ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) iliyokuwa kwenye anga hilo kwa ajili ya matengenezo na kubaini jumla ya lita 220 ndizo zilizoibiwa kutoka kwenye ndege ya kampuni hiyo.
Kuhusu taarifa ya kikosi cha usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 17.03.2017 hadi Tarehe 21.03.2017 wamekusanya jumla ya shilingi 432,990,000 kutokana na makosa ya barabarani.
Kuhusu tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji Clouds Kamishna Sirro amesema amelisikia suala hilo lakini bado ripoti ya tukio hilo haijafikishwa rasmi ofisini kwake na pindi ripoti hiyo itakafika ofisini kwake atachukua hatua za kisheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni