Rais Magufuli amempongeza Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma kwa utendaji kazi wake.
Rais Magufuli amesema, ''Pamoja na kwamba CCM tuliteleza kidogo lakini Mbunge huyu ni mchapakazi kweli''.
Aliendelea kusema, ''Tunahitaji Wabunge wa aina hii, tumezunguka naye
katika ziara yangu na kujionea kazi zake anazozifanya, Yeye anataka
maendeleo ya wananchi wake''.
Alimalizia kwa kusema, ''Kwa kweli ninakupongeza, hongera sana. Una moyo mzuri hata sura nzuri''.
''Inawezekana sura ikawa CUF CUF lakini moyo wake ni CCM, Ningetamani siku moja ukahamia CCM, ningefurahi sana'' alisema Rais.
Mbunge Maftaha alimshukuru Rais kwa kumpa ushirikiano wa karibu katika kazi zake za kuwatumikia wananchi wa Mtwara Mjini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni