STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ambaye alikuwapo mkoani Arusha
kwa ajili ya kumsabahi Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anadaiwa
kuwa mjamzito kwa sasa.
Uvumi huo umeanza baada ya kuzagaa picha za mrembo huyo aliyewahi kutwaa
taji la Miss Tanzania mwaka 2006 kwenye kurasa mbalimbali za mitandao
ya kijamii.
Picha hizo ambazo zilimwonyesha Wema akiwa na tumbo lenye ukubwa kiasi,
zilizua shangwe kwa mashabiki wake wakiamini mrembo huyo huenda akawa na
ujauzito.
Pamoja na maswali mengi ya mashabiki wake, Wema hakuweza kujibu chochote
kuhusu madai hayo na kuwafanya wale wote wanaomuunga mkono, yaani ‘Team
Wema’ kuendelea wakizituma picha hizo kwenye kurasa zao za mitandao ya
kijamii.
Lakini jambo kubwa lililozidi kuwachanganya mashabiki wake ni ujumbe
tata wa Idrisa Sultan ambaye ni mpenzi wa zamani wa Wema ambaye
aliandika: “Pigo moja tu, mbuyu chini.” Ujumbe uliozidi kuwaweka
njiapanda mashabiki wa mkali huyo wa filamu.
Wema amekuwa kwenye kilio cha muda mrefu kutafuta mtoto, ambapo amewahi
kubeba ujauzito wa mapacha wawili lakini haukuweza kudumu baada ya
kutoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni