Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Miss Tanzania 2006 Wema
Sepetu ameshiriki kwa kupanda miti katika vyanzo vya maji vya Mbogo na
Nukutu katika milima ya Uluguru, Manispaa ya Morogoro.
Wema akiwa ameungana na baadhi ya viongozi akiwemo Devotha Minja. |
Wema aliyeungana na Mbunge wa Viti
Maalum mkoa wa Morogoro kupitia CHADEMA, Devotha Minja, Diwani wa kata
hiyo pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa, wamefikia hatua hiyo kwa
lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa vikiharibiwa kwa
kiasi kikubwa katika maeneo hayo, hali inayotishia maisha ya viumbe
pamoja na wakazi wanaotegemea vyanzo hivyo.
Mrembo huyo ambaye pia msanii wa filamu
nchini, amesema kuwa ameamua kuunga mkono jitihada hizo za kuhifadhi
vyanzo vya maji ili kuondoa kero za maji ambazo wanawake hukumbana nazo,
huku akitoa somo kuwa faida na manufaa ya miti hiyo zitaonekana
baadaye.
Zoezi la kupanda miti likiwa linaendelea. |
"Jana ilikuwa siku ya wanawake
duniani, nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro
siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa na tija kwetu na
kupunguza kero kubwa inayotukabiri ya maji, wote tunajua kuwa mwanamke
ndiyo anakerwa zaidi katika upatikanaji wa maji labda haittusaidia leo
wala kesho lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu vya baadae". Amesem Wema Sepetu.
Wema ambaye hivi karibuni ametangaza
kujiunga na CHADEMA akitokea CCM, amesema ameongeza kuwa mazingira
hayana itikadi wala vyama na kwamba yanamgusa kila mtu hivyo yampasa
kila mmoja kupanda miti ili kuweza kulinda vyanzo vya maji.
Mh. Devotha Minja akizungumzia umuhimu wa kuhifadhi mazingira hususani katika milima ya Uluguru
Kwa upande wake Mbunge Devotha Minja
ambaye kabla ya kuwa mbunge amekuwa akiripoti habari nyingi kuhusiana na
uharibifu wa mazingira kupitia kazi yake ya uandishi wa habari, amesema
ameamua kuchukua hatua kwa vitendo kama kiongozi ili kuwa mfano kwa
jamii nzima ya watanzania hususani wakazi wa Morogoro, kuhusu umuhimu wa
kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni