FOR ADVERTISE PLEASE CONTACT US THROUGH E-mail; msetoperfecttz@gmail.com OR 255 717 338 243

Jumapili, 5 Machi 2017

YANGA UBINGWA WA KUSUA SUA MSIMU HUU

Klabu ya Yanga imeshindwa kuishusha klabu ya Simba kileleni mwa Ligi Kuu Bara leo baada ya timu hiyo kulazimisha droo ya bila kufungana na klabu ya Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro. 
 
PICHANI: MECHI KATI YA YOUNG AFRICAN SC NA MTIBWA SUKARI


Katika mchezo ambao umewakutanisha Simba na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri Morogoro, Yanga ilianza vyema kwa kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hayakuweza kuleta mafanikio kwa klabu hiyo, Yanga walifanikiwa kupata penati ambayo ilipigwa na Saimon Msuva lakini mchezaji huyo alipaisha penati hiyo na kufanya mpaka mpira unakwisha katika kipindi cha kwanza timu hizo zikitoka bila kufungana.
Katika dakika 45 za kwanza za mchezo Yanga iliweza kuongoza kumiliki mpira kwa asilimia 54 huku Mtibwa Sugar ikimiliki mpira kwa asimilia 46.
Katika kipindi cha pili timu zote zilionyesha uwezo na nia ya kutafuta mabao lakini jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda kwa klabu zote mbili na kufanya klabu ya Mtibwa Sugar kumiliki mpira kwa asilimia 55 dhidi ya Yanga ambao walimiliki mchezo kwa asilimia 45 kwa kipindi chote cha mchezo.
Baada ya mpira kumalizika Nahodha wa Mtibwa Sugar Shabani Nditi alifunga na kusema timu yao inamapungufu kwenye ufungaji jambo ambalo mwalimu amekuwa akiendelea kulifanyia kazi, huku Nahodha wa Yanga Cannavaro akiwapongeza Mtibwa Sugar kwa mchezo wao lakini amewataka mashabiki wa Yanga kutokata tamaa kwani bado nafasi wanayo kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
"Nawapongeza Mtibwa Sugar na timu yangu pia kwa kucheza vizuri, tumetengeneza nafasi nyingi ikiwepo penati lakini huu ndiyo mpira, bado tuna nafasi kubwa kutetea ubingwa ingawa ligi sasa ni ngumu ila mashabiki wasikate tamaa mechi sita bado ndefu na bado tunanafasi ya kufanya vyema" alisisitiza Cannavaro
Mpaka sasa Simba inaongoza Ligi Kuu bara kwa kuwa na pointi 55 ikifuatiwa na Yanga ambayo sasa ina pointi 53.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni