Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni mwanaharakati
wa masuala ya vijana, Dkt. Hamis Kigwangalla ameshindwa kujizuia na
kufunguka jinsi anavyomuhusudu mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz
Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Nzega, ametumia ukurasa wake wa twitter kutamka rasmi kuwa hajawahi
kuwa shabiki wa Diamond, lakini kazi zake anazikubali hasa zile
zilizokaa kimikakati ya biashara.
"Sikuwahi kuwa mshabiki wa Diamond
Platnumz, japokuwa ni mwimbaji mzuri, ila nakubali sana kipaji chake
kwenye 'biashara' ya muziki" Amesema Kigwangalla
Ametaja ngoma iliyomfanya aanze
kumkubali tena Diamond, mbali na ile ya Mbagala, kuwa ni Marry You
aliyoshirikiana na Ne-Yo kutoka nchini marekani.
"Zaidi ya nyimbo ya Diamond Platnumz
Mbagala (ambayo naipenda mpaka kesho), na juzi hapa nyimbo za Ngololo,
Salome, hii ya Marry You" Aliandika Kigwangalla
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni