Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania (Kamati ya
Saa 72), imeipiga klabu ya Yanga faini ya shilingi 500,000 kufuatia
kutumia mlango usio rasmi katika mechi yake dhidi ya Simba iliyopigwa
terehe 25, mwezi Februari.
Adhabu hiyo imetolewa katika kikao chake
cha Machi 4, 2017 iliptia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2016/2017 inayoendelea hivi sasa.
Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo
imesema kuwa, katika mchezo kati ya Simba na Young Africans iliyochezwa
Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Young
Africans iliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
"Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha
kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani
kwa kutumia milango rasmi, Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya
Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini
tano)." Imesema taarifa hiyo
Kikao hicho pia kilifuta kadi ya kwanza
ya njano aliyoadhibiwa mchezaji Obrey Chirwa wa Young Africans wakati
timu hiyo ilipocheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi
mosi, mwaka huu na hivyo kufuta kadi nyekundu aliyoadhibiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni