Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
ameachiwa kwa dhamana (ya polisi) iliyowekwa na wanasheria wawili,
Hekima Mwasipu na Nashon Nkungu baada ya kushikiliwa na polisi kwa saa
kadhaa leo.
Picha: Maktaba (Lissu akitoka mahakamani hivi karibuni baada ya kupata dhamana katika kesi nyingine inayomkabili |
Lissu
alikamatwa ghafla leo alipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
baada ya mashitaka yake ya uchochezo katika moja ya kesi zinazomkabili,
kufutwa.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Lissu alikamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za
kutoa maneno ya uchochezi ambayo yangeweza kuibua mtafaruku wa kidini
katika jamii wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi
mdogo Jimbo la Dimani, Zanzibar, mwezi Januari mwaka huu.
Baada ya mahojiano ya leo, Lissu
ameachiwa kwa sharti la kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Machi 13, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni