Je unazijuwa kazi za maji mwilini? Au ukishakunywa tu na kiu kukatika
basi unakuwa huelewi nini kinaendelea baada ya hapo. Mashuleni umhimu wa
maji mwilini unafundishwa kwa kiasi kidogo sana na mara nyingi maji ya
kunywa yamefundishwa au kuchukuliwa kuwa ni kitu cha kusafirishia viini
lishe toka sehemu moja au nyingine tu. Lakini maji yana umhimu mkubwa mwilini zaidi ya hapo.
Tunaposema maji ni uhai huenda unaichukulia kauli hii kirahisirahisi tu,
lakini leo utajuwa ni kwanini maji yaliitwa ni uhai. Endelea kusoma.
Baada ya oksijeni, maji ndicho kitu pekee ili kuishi. Zifuatazo ni baadhi ya KAZI 41 mhimu ZAIDI za maji mwilini kama ifuatavyo:
1. Bila maji hakuna kinachoishi. Wakati wowote unapopungukiwa maji, baadhi ya seli zako ndani ya mwili hufa.
2. Panapotokea upungufu wa maji, kitu kimoja lazima kipotee, baadhi ya kazi za seli hufa.
3. Maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu, maji ndiyo hela ya mwili, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
4. Maji hutumika kama moja ya malighafi katika usanifu na ujenzi wa seli, huziweka seli pamoja.
5. Maji hukinga uharibifu wa vinasaba (DNA), Vinasaba vichache visivyo vya kawaida huzarishwa.
6. Maji kwa uwezo mkubwa yanaongeza uwezo, nguvu na kinga ya mwili, ujuzi huu wote unahusisha pia dhidi ya kansa.
7. Maji ni wakala mhimu katika mmeng’enyo wa vyakula karibu vyote, vitamini na madini.
8. Maji yanatumika kusafirisha vitu vyote mwilini, maji yanapoifikia
seli, huipa pia oksijeni na kuchukuwa hewa chafu hadi kwenye mapafu ili
kutolewa nje ya mwili.
9. Maji huzisomba taka chafu toka sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye Ini na Figo ili kutolewa nje.
10. Maji ni mhimu ili kulainisha sehemu zote za mwili, hivyo kuzuia kufunga choo.
11. Maji huzuia shambulio la moyo na mshituko.
12. Maji ni mhimu katika kuupooza na kuupa mwili joto.
13. Nguvu za kiumeme katika maji hutupa nguvu za kufikiri, kufikiri kunahitaji nguvu, hivyo kuhitaji maji.
14. Maji ndicho kiamusho au kichangamusho (pick-me-up) pekee bora cha
miili yetu kuliko kinywaji kingine chochote duniani, bila madhara.
15. Maji yatakurudishia usingizi wa kawaida na mororo, kila tuotapo
ndoto mbaya au za kutisha (nightmares), mwili huwa unatuamusha kwenda
kunywa maji. Jaribu hii, siku yeyote ukiota ndoto ya kutisha, amka na
kunywa glasi moja ya maji kisha rudi kulala.
16. Maji huzuia uchovu, huwapa vijana nguvu. Fikiri: unapokuwa na uchovu
na ukaamua kuoga, baada ya kuoga sehemu kubwa ya uchovu hupotea. Hapo
umeoga tu, je ukiyanywa maji yenyewe?!!.
17. Maji hutengeneza ngozi nyororo hivyo kuzuia kuzeeka mapema.
18. Maji yatausawazisha katika hali yake ya kawaida mfumo wa uzarishaji damu kwenye mifupa, hivyo kuzuia Leukemia na Anaemia.
19. Maji yatapunguza maumivu ya ishara za kutokea kwa hedhi.
20. Upungufu wa maji mwilini huzuia uzarishwaji wa homoni za kiume na
kike, hii ndiyo sababu ya kwanza ya uhanithi (impotence) na kukosa hamu
ya tendo la ndoa (negative sex libido). Kuna tatizo kubwa linaendelea
kwenye jamii yetu la upungufu wa nguvu za kijinsia hasa upande wa kina
baba na kwa sehemu kubwa ni matokeo ya upungufu wa maji na chumvi
mwilini.
21. Kunywa maji kutakutofautishia hisia za njaa na kiu ya maji, kunywa
maji kwa muda na upunguze uzito na unene bila kuacha kula (dieting).
22. Maji yatazuia homa za asubuhi kwa mama mjamzito.
23. Maji yataunganisha mawazo na kazi za mwili, yataongeza uwezo katika kutambua malengo na nia.
24. Maji yatageuza utegemezi kwa vilevi ikiwa ni pamoja na pombe, kafeina na baadhi ya madawa ya kulevya.
25. Maji huzarisha nguvu za kiumeme na nguvu za kisumaku katika kila
seli ya mwili – nguvu za kuishi. Nguvu za kiumeme zinafanya kazi kama
nguvu za kisumaku na kuvipanga vitu anuwai kama sumaku hivyo kutoa uwepo
wake sahihi na kujihusisha na matendo ya kikemikali.
26. Maji yanatumika katika kuvikatakata vyakula kuwa vipande vidogovidogo na hatimaye umetaboli au umeng’enywaji wake.
27. Maji yatakiongezea nguvu chakula (yaani maji ni transfoma chocheo ya
chakula) na hatimaye chakula kutoa nguvu kwa mwili wakati wa
umeng’enywaji wake.
28. Maji yataongeza uchukuwaji wa viini lishe mhimu vilivyomo kwenye
chakula. Hii ina maana gani? Ni hivi, unapokula chakula na hauna maji ya
kutosha mwilini basi ni viinilishe vichache tu ndivyo vitachukuliwa na
mwili wakati sehemu nyingine kubwa ya chakula itabaki kama takataka tu.
29. Maji ni kilainishi kikuu kwenye maeneo ya maungio (joints) na hivyo kuzuia ugonjwa wa yabisi na kupooza.
30. Maji hutumika kwenye ‘diski’ za uti wa mgongo kuzifanya zigongane na kufyonza maji.
31. Maji huzuia kuzibika (clogging) kwa ateri kwenye moyo.
32. Maji huzuia kupunguwa kwa umakini na usikivu kwa watoto na watu wazima (Attention deficit disorder – ADD).
33. Maji huongeza ufanisi katika kazi.
34. Maji yatazuia mfadhaiko, pupa na kukata tamaa.
35. Maji huzuia ugonjwa wa Glakoma.
36. Maji yataiyeyusha damu na kuizuia isigande wakati wa mzunguko wake.
37. Upungufu wa maji unavihifadhi vijidudu nyemelezi (free radicals)
mwilini, na maji ndiye muondoaji mkuu wa vijidudu hivi nyemelezi.
38. Maji hutoa nuru na mng’aro kwa macho na kuhimili kuona kwa sababu
kushughulika na taarifa za mwanga kunahitaji nguvu nyingi katika
kusafirisha taarifa toka mfumo mmoja katika jicho kwenda katika mfumo
mwingine kwenye ubongo ili kutafusiriwa.
39. Maji na mapigo ya moyo vinatengeneza muyeyuko na mawimbi ili kuzuia vitu visivyotakiwa kubaki kwenye mkondo wa damu.
40. Mwili wa binadamu hauna hifadhi (store) ya maji, ndiyo maana unatakiwa kuyanywa kila siku.
41. Kunywa maji halisi, safi na salama kwa kanuni sahihi, kunausafisha
mwili, maji yanaiacha sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (colon) kuwa na
uwezo zaidi wa kutengeneza damu mpya (fresh blood) ijulikanayo katika
lugha ya kitaalamu kama ‘Haematopaises’, kwamba difu la utumbo mkubwa na
utumbo mdogo (mucousal fold) huamushwa upya kwa njia hii.
Ifike mahala tuache mazoea ya kuipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni