Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli ametoa
agizo kwa uongozi wa tanesco kukata umeme kwa Wizara au taasisi yoyote
inayokwepa kulipa bili za umeme.
Mh Rais ameyasema hayo leo katika ziara yake ya kuzindua na kuweka jiwe
la msingi katika mradi wa umeme wa msongo wa Kv 132 Mtwara " Tanesco
pasitokee taasisi ama Wizara hata Ikulu isipolipa umeme we kata tu,
hatuwezi kujiendesha kwa hasara wakati kuna watu wanakwepa kulipia
gharama" wakati serikali inatoa ruzuku zake humu sasa ni wakati Tanesco
ijiendeshe kwa faida.
Aidha Mh Rais ameonya tanesco kutoingia mikataba ya hovyo na makampuni
ya nje yanayokuja kwa ujanja na alisema kampuni ikitaka kuja kuwekeza
umeme nchini basi waje wazalishe umeme wao na wauze tanesco na
wasitegemee umeme huu kufanya ujanja ili kutorudia mikataba mibovu kama
symbion na makampuni mengine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni