FOR ADVERTISE PLEASE CONTACT US THROUGH E-mail; msetoperfecttz@gmail.com OR 255 717 338 243

Alhamisi, 2 Machi 2017

Mambo 8 TWAWEZA wameyataja kuhusu upungufu wa chakula Tanzania

Miezi kadhaa iliyopita kumekuwepo na mijadala mizito ya kisiasa na kitaifa juu ya upungufu wa chakula Tanzania. Taaarifa za upungufu wa chakula mwanzoni zilikataliwa na viongozi wa juu wa serikali lakini baadae walikiri kuwepo kwa tatizo hilo nchini.
Mwishoni mwa mwezi Januari 2017, Waziri wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba aliliambia bunge kwamba utafiti uliofanywa na Wizara kwa kushirikiana na wadau kadhaa, umegundua kwamba Wilaya 55 (kati 169 za Tanzania Bara na Visiwani) zilikumbwa na njaa.
Taarifa yake ilieleza kuwa tani 35,491 za nafaka zinahitajika kusambazwa kati ya mwezi wa pili na wa nne mwaka 2017 ili kukabiliana na upungufu huo uliowakumba watu 1,186,028”2 katika Wilaya hizo.
Leo March 1, 2017 Ripoti mpya ya taasisi ya utafiti ya Twaweza imetoa matokeo ya utafiti wake uliofanywa nchini ili kubaini ukweli wa suala la upungufu wa chakula.
Nimekuwekea hapa mambo nane yaliyobainika kwenye utafiti wa TWAWEZA.
 Wananchi 9 kati ya 10 wanaona ni jukumu lao kuhakikisha wana fedha za kutosha ili kukidhi mahitaji ya kaya zao.

Kpindi cha mwaka mmoja uliopita kaya moja kati ya 8 imepokea fao, faida au pesa kutoka ktk miradi ya serikali


  Kpindi cha mwaka mmoja uliopita kaya moja kati ya 8 imepokea fao, faida au pesa kutoka ktk miradi ya serikali.Kaya 8 kati ya 10 (79%) zimeripoti kwamba zinahifadhi chakula kwa ajili ya dharura au kuepukana na njaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni