FOR ADVERTISE PLEASE CONTACT US THROUGH E-mail; msetoperfecttz@gmail.com OR 255 717 338 243

Jumapili, 5 Machi 2017

MASHABIKI WA YANGA WANA KELELE SANA - AUNTY EZEKIEL


Msanii wa filamu nchini Aunty Ezekiel amefunguka na kusema kuwa mashabiki wa Yanga siku zote wamekuwa na makelele sana hasa zaidi wanaposhinda mechi zao jambo ambalo linafanya timu hiyo kuendelea kuwa mteja kwa Simba. 

Aunty Ezekiel alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane kamili mchana mpaka saa kumi jioni.
"Mimi toka nakua ukisikia Simba na Yanga lazima Simba ashinde yaani ni mara chache sana Yanga ndiyo huwa wanashinda labda ni Mungu tu huwa anapanga maana Yanga wakishinda huwa wanakuwa na kelele sana kwa hiyo vile vitu Mungu hapendi, ndiyo maana mara nyingi Yanga wanashindwa, Yanga hawashindi kwa sababu ya kelele zao kwa hiyo wapunguze kelele Mungu anaweza kuwaangalia kwa namna nyingine" alisema Aunty Ezekiel

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni