Wema Sepetu akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye hivi sasa amehamia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametimiza hadi yake kwenda kuonana na
Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema ambaye amepata dhamani siku ya
Ijumaa na kutoka gerezani.
Wema Sepetu juzi alisema atakwenda Arusha kuonana na Mbunge huyo ambaye
amekaa ndani kwa zaidi ya miezi mitatu na kusema ni faraja kwao saizi
kuona ametoka na kuja kuendeleza mapambano
"Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano, kwenye
mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono
mpaka kieleweke. For that sake, kesho (jana) i'll be in Arusha kuonyesha
Solidarity" alisema Wema Sepetu
Baada ya Wema Sepetu kufanikiwa kuonana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema
amefunguka na kusema saizi anajisikia furaha na amani kuwa ndani ya
chama hicho
"Finally Met my brother, aisee Chadema inanipa furaha mimi. Nina amani
ya moyo... Ona Venye nacheka .... It was A Good Day...." aliandika Wema
Sepetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni