MSETOPERFECT TZ

FOR ADVERTISE PLEASE CONTACT US THROUGH E-mail; msetoperfecttz@gmail.com OR 255 717 338 243

RECENT POST

Jumatano, 22 Machi 2017


Kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa ya mfumo wa mkojo (UTI) na uzazi kwa wanawake, hii inasababishwa na sababu nyingi ikiwemo ya kukosa uelewa sahihi wa kanuni za afya na usafi wa mwili pamoja na mazingira yanayomzunguka mwanamke. 
Mada za usafi wa mwanamke ni pana sana siwezi kumaliza kusema kila kitu, hivyo leo nitajikita zaidi katika matumizi sahihi ya pedi na mambo ya kuzingatia kabla ya kunua pedi. Wadada wengi wamekuwa wakitumia pedi na kuziacha zikizagaa mitaani hali inayofanya nijiulize kama tu ameshindwa kujua sehemu sahihi ya kuhifahi au kutupa pedi aliyotumia yeye mwenyewe, 
Je anauelewa upi katika matumizi sahihi ya pedi hizo kabla hajazitumia?
 Somo la leo nitajikita katika njia sahihi ya kuchagua na kutumia pedi, makosa yanayofanywa katika matumizi ya pedi na ushauri juu ya matumizi sahihi ya pedi na vitambaa kwa wale wanaovitumia.

Yafuatayo ni makosa yanayofanywa katika uchaguzi na matumizi ya pedi kwa wanawake:

1. Kutonawa mikono kabla na baada ya kutumia pedi. Mikono hushika sehemu mbalimbali hivyo kuna uwezekano ikawa na vimelea vinavyosababisha magonjwa kwa hiyo kushika pedi bila kunawa mikono kwa sabuni kunaweza kuhamisha vimelea hivyo kutoka mikononi na kwenda kwenye pedi inayotegemewa kuvaliwa.

2. Kutunza pedi bafuni au chuoni. Wadada wengi hupendelea kutunza pedi zao chooni/bafuni. Vyumba vingi vya choo/bafu havina mwanga wa kutosha na kuwa na unyevunyevu hali inayoweka mazingira mazuri ya ukuaji wa vimelea vya magonjwa kama bacteria na kitendo cha kutunza pedi katika sehemu hizo kunaweza kusababisha kuhama kwa vimelea hao kutoka bafuni/chuoni kwenda kwenye pedi isiyovaliwa na kupelekea pedi hizo kuwa na vimelea vya magonjwa na mwanamke anakuwa katika hatari za kupata maambukizi.

3. Kutoangalia muda wa matumizi wa pedi kabla ya kutumia au baada ya kuzihifadhi kwa muda mrefu hali inayopunguza kiwango cha ufanisi cha pedi sababu ya kuisha kwa muda wake wa matumizi.

4. Kununua pedi zinazouzwa kiholela kwa njia ya utangazaji na za bei rahisi (promotion) ambazo baadhi zimeonekana kutengenezwa kwa malighafi zilizo chini ya kiwango au kukaa kwa muda mrefu hivyo kuuzwa kwa bei rahisi ili zitoke na kutumika haraka kabla ya kuisha muda wake.

5. Kutumia pedi ambazo zipo katika majaribio maalum. Kama tunavyojua kuna kila aina za pedi mpya katika soko kwa kadri siku zinavyozidi kwenda na baadhi ya pedi huingizwa sokoni kinyemela pasipo tafiti za kutosha na bila hata kuthibishwa na mamlaka husika.

6. Kutumia pedi kwa muda mrefu. Wanawake wengi hususani katika nchi zinazoendelea huwa hawamudu kutumia pedi moja kwa muda wa masaa mawili kama inavyoshauriwa na wataalamu hivyo kujikuta katika hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa mkujo na njia za uzazi .

7. Kupendelea pedi zenye uwezo mkubwa wa kufyonza unyevunyevu ili ivaliwe muda mrefu pia ni tatizo sababu kwa kadri muda wa kuvaa pedi moja unapozidi kuongezeka na hatari za maambukizi ya magonjwa pia inazidi kuongozeka.

Wanawake wanashauriwa kufanya yafuatayo ili kuhakikisha usalama wa afya zao :

1. Kunawa mikono vizuri kwa sabuni kabla ya kugusa pedi ambayo unatarajia kuivaa na baada ya kuvaa kunawa tena mikono vizuri.

2. Kutohifadhi pedi bafuni au chuoni au sehemu yote yenye unyevunyevu na isiyo na mwanga wa kutosha ili kutotengeneza mazingira ya kukua kwa vimelea vya magonjwa ndani ya pedi.

3. Kuangalia kwa makini muda wa matumizi ya pedi kabla ya kununua au baada ya kutunza pedi kwa muda muda mrefu ili kuepuka kutumia pedi zilizopita muda wake wa matumizi.

4. Kuepuka kununua pedi zinazouzwa kiholela na zisizothibitishwa na TBS na mamlaka nyingine zenye dhamana ya kuangalia ubora wa pedi hizo. Mwanamke anatakiwa kuangalia nembo ya uthibitisho wa mamlaka hizo na kujiridhisha kuhusiana na usalama wa pedi hizo kabla hajanunua.

5. Kubadilisha pedi kila baada ya masaa mawili, kama tunavyojua damu ni moja wapo ya chakula kizuri sana kwa vimelea vya magonjwa kama bacteria ,unyevunyevu unaosababishwa na kuvaa pedi kwa muda mrefu pia unapelekea ustawi wa bacteria hao na joto ambalo lipo katika maumbile ya ndani ya mwanamke vikiungana kwa pamoja vinatengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa bacteria , hivyo wanawake wanashauriwa kutovaa pedi hizo kwa muda usiozidi masaa mawili ili kuepuka mazingira hayo.

6. Kuchagua aina sahihi inayokutosha ina kuepuka pedi zinazobana sana kupita kiwango sababu zinaweza pia kukufanya usiwe huru na kutengeneza joto la ziada na michubuko katika maumbile ya mwanamke,hivyo mwanadada unashauriwa kutumia pedi itakayokukaa vizuri(isilegee sana wala kuachia sana)

7. Kwa wadada wanaotumia vitambaa badala ya pedi ni muhimu pia kuzingatia kanuni za kiafya na usafi kabla na baada ya kutumia vitambaa hivyo kama vile kuchagua kitambaa angavu ,kukiloweka na kukifua vizuri, kuanika kwenye sehemu yenye mwanga wa jua wa kutosha na upepo wa kutosha pasipo na unyevunyevu ,kupiga pasi kabla ujakihifadhi na kabla ya kutumia ili kuuwa vimelea vya magonjwa na kuvitunza sehemu nzuri ambayo haina unyevunyevu, penye hewa na mwanga wa kutosha na mwisho ni kubadilisha kitambaa hicho kila baada ya masaa mawili pamoja na kunawa mikono vizuri kabla na baada ya matumizi ya vitambaa hivyo.
Continue reading

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na wizi, uuzaji na ununuzi wa mafuta ya ndege nchini.
Kamanda wa kanda maalumu afande Kamishna Simon Sirro
Kamishna Sirro ametoa onyo hilo leo jijini Dar es Salaam baada ya kumkamata mttu mmoja aitwae Iddy Juma Nyangasa mkazi wa Vingunguti baada ya kuiba lita 38 za mafuta ya ndege kutoka kwenye ndege mali ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) iliyokuwa kwenye anga hilo kwa ajili ya matengenezo na kubaini jumla ya lita 220 ndizo zilizoibiwa kutoka kwenye ndege ya kampuni hiyo.
Kuhusu taarifa ya kikosi cha usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 17.03.2017 hadi Tarehe 21.03.2017 wamekusanya jumla ya shilingi 432,990,000 kutokana na makosa ya barabarani.
Kuhusu tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji Clouds Kamishna Sirro amesema amelisikia suala hilo lakini bado ripoti ya tukio hilo haijafikishwa rasmi ofisini kwake na pindi ripoti hiyo itakafika ofisini kwake atachukua hatua za kisheria.
Continue reading

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amedaiwa kuwatishia kuwafunga jela miezi 6 au kuwapa tuhuma za dawa za kulevya bila kupitia mahakamani wafanyakazi wa kituo cha utangazaji cha Clouds kwa kukataa kurusha habari aliyoitaka.
Waziri Nape Nnauye (kulia) akipokea taarifa ya uchunguzi kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati, Hassan Abas
Hayo yamebainika katika ripoti ya uchunguzi wa tukio la mkuu huyo wa mkoa kuvamia katika kituo cha utangazaji cha Clouds akiwa na askari wenye silaha, ripoti ambayo pia imependekeza mamlaka husika kumchukulia hatua za kinidhamu.
Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mbele ya wanahabari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Kamati ya uchunguzi Deodatusi Balile amesema kamati hiyo haikuweza kumpata Paul Makonda kwa ajili ya mahojiano.
Akitaja mambo yaliyobainika katika sakata hilo, Balile amesema kamati hiyo iliyohoji watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi 14 wa kituo cha Clouds, imejiridhisha pasipo shaka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alivamia katika kituo hicho saa 4:30 usiku wa Machi 17 akiwa anaendesha gari yenye namba za usajili T553 BFH.
Amesema uchunguzi wa kamati umebaini kuwa sababu ya uvamizi huo ni habari iliyodaiwa kumuhusu mwanamke aliyedai kuzaa na Mchungaji Josephati Gwajima ambapo alitaka habari hiyo iruke kwenye kipindi..
Pia kamati hiyo imethibitisha kuwa Makonda na askari waliingia hadi katika vyumba ambavyo hawakupaswa kuingia, na waliingia hadi kwenye studio ambayo inarusha matangazo na kutoa vitisho kwa watangazaji, waandaji na wafanyakazi wengine, kiasi cha baadhi yao kuagua vilio.
“Vitisho hivyo ni askari wenye silaha za moto, kuingia ndani ya studio kibabe wakiwa na silaha za moto, Makonda aliwatisha usiku huo kwamba angewafunga jela miezi sita, pia angewakagua watangazaji wa kipindi kama wanahusika na dawa za kulevya, au kuwabana wadhamini wa kipindi na pengine kuwaingiza kwenye orodha ya wahusika wa dawa za kulevya endapo wangeendelea na msimamo wao” Amesema Balile
Deodatusi Balile akisoma taarifa hiyo
Pia amesema kamati imebaini kuingiliwa kwa uhuru wa habari kinyume cha sheria kwa kulazimisha kutangazwa kwa habari isiyokidhi vigezo.
Kuhusu wafanyakazi kupigwa, Balile amesema kamati hiyo haikuona uthibitisho wowote kuwa kuna watu walipigwa, isipokuwa wapo waliolia kutokana na vitisho vya kupelekwa jela miezi 6.
Kamati hiyo imetoa mapendekezo manne ikiwa ni pamoja kumtaka Makonda aombe radhi kwa tasnia ya habari, kumtaka Waziri kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka yake ya uteuzi ili hatua zichukuliwe, vyombo vya dola vianzishe uchunguzi wa ndani dhidi ya askari walioingia.
Amesema kamati hiyo ilijirisha kuwa Makonda hakuwa tayari kuhojiwa wala kutumia fursa ya kujieleza jambo ambalo hata hivyo halikuathiri uchunguzi wa kamati hiyo.
"Tulianza kwa kumpigia simu, lakini hakupokea, tukaamua kumpelekea ujumbe hakuujibu, tukatumia wasaidizi, wakatutaka tufike ofisini kwake, tulifanya hivyo, tulifika lakini ilielezwa kuwa ana mgeni, ulipofika muda akatuita, tukaelekezwa kupita ngazi za mbele lakini yeye akapita mlango wa nyuma akaondoka. Tukaambiwa tumsubiri, tukasubiri lakini baadaye tukaambiwa amepata shughuli nyingine kwa hiyo hataweza kurejea ofisini". Amesema Balile
Waziri Nape (Kushoto) na Balile
Mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Waziri Nape amesema ataifikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya hatua kuchukuliwa huku akiwataka wanahabari kuendelea kuwa na imani na serikali katika kulinda uhuru wa habari.
"Juu yangu kuna Waziri Mkuu, kuna Makamu wa Rais na kuna Rais, nitawakabidhi ripoti hii, nawaomba wanahabari, tuendelee kuwa watulivu, Rais wetu Magufuli ana nia njema na tasnia ya habari na ndiyo maana akaipitisha haraka sheria inayoipa hadhi tasnia hii... Wakati mwingine madhaifu yakitokea kwa mtendaji mmoja mmoja, yasiwe tope kwa serikali nzima....Mimi nitaipeleka taarifa kwa wenzangu, wataiangalia na litakuwa ni funzo kwa watu wengine" Amehitimisha Waziri Nape
Continue reading

Alhamisi, 9 Machi 2017

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ameshiriki kwa kupanda miti katika vyanzo vya maji vya Mbogo na Nukutu katika milima ya Uluguru, Manispaa ya Morogoro. 
Wema akiwa ameungana na baadhi ya viongozi akiwemo Devotha Minja.

Wema aliyeungana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Morogoro kupitia CHADEMA, Devotha Minja, Diwani wa kata hiyo pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa, wamefikia hatua hiyo kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa vikiharibiwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo hayo, hali inayotishia maisha ya viumbe pamoja na wakazi wanaotegemea vyanzo hivyo.
Mrembo huyo ambaye pia msanii wa filamu nchini, amesema kuwa ameamua kuunga mkono jitihada hizo za kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuondoa kero za maji ambazo wanawake hukumbana nazo, huku akitoa somo kuwa faida na manufaa ya miti hiyo zitaonekana baadaye.
Zoezi la kupanda miti likiwa linaendelea.
"Jana ilikuwa siku ya wanawake duniani, nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa na tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabiri ya maji, wote tunajua kuwa mwanamke ndiyo anakerwa zaidi katika upatikanaji wa maji labda haittusaidia leo wala kesho lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu vya baadae". Amesem Wema Sepetu.

Wema ambaye hivi karibuni ametangaza kujiunga na CHADEMA akitokea CCM, amesema ameongeza kuwa mazingira hayana itikadi wala vyama na kwamba yanamgusa kila mtu hivyo yampasa kila mmoja kupanda miti ili kuweza kulinda vyanzo vya maji.
Mh. Devotha Minja akizungumzia umuhimu wa kuhifadhi mazingira hususani katika milima ya Uluguru
Kwa upande wake Mbunge Devotha Minja ambaye kabla ya kuwa mbunge amekuwa akiripoti habari nyingi kuhusiana na uharibifu wa mazingira kupitia kazi yake ya uandishi wa habari, amesema ameamua kuchukua hatua kwa vitendo kama kiongozi ili kuwa mfano kwa jamii nzima ya watanzania hususani wakazi wa Morogoro, kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Continue reading










































Continue reading

Jumatano, 8 Machi 2017


STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ambaye alikuwapo mkoani Arusha kwa ajili ya kumsabahi Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anadaiwa kuwa mjamzito kwa sasa.
Uvumi huo umeanza baada ya kuzagaa picha za mrembo huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006 kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.
Picha hizo ambazo zilimwonyesha Wema akiwa na tumbo lenye ukubwa kiasi, zilizua shangwe kwa mashabiki wake wakiamini mrembo huyo huenda akawa na ujauzito.
Pamoja na maswali mengi ya mashabiki wake, Wema hakuweza kujibu chochote kuhusu madai hayo na kuwafanya wale wote wanaomuunga mkono, yaani ‘Team Wema’ kuendelea  wakizituma picha hizo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Lakini jambo kubwa lililozidi kuwachanganya mashabiki wake ni ujumbe tata wa Idrisa Sultan ambaye ni mpenzi wa zamani wa Wema ambaye aliandika: “Pigo moja tu, mbuyu chini.” Ujumbe uliozidi kuwaweka njiapanda mashabiki wa mkali huyo wa filamu.
Wema amekuwa kwenye kilio cha muda mrefu kutafuta mtoto, ambapo amewahi kubeba ujauzito wa mapacha wawili lakini haukuweza kudumu baada ya kutoka.
Continue reading